Ni School Management System inayofanya mambo yafuatayo:
1.Inamuwezesha mwalimu wa somo kurekodi na kutunza alama za majaribio na mitihani wanayofanya wanafunzi anaowafundisha. Mfumo una mazingira mazuri yanayomuwezesha mwalimu kuingiza alama kwa haraka bila kujali idadi na mpangilio wa karatasi za wanafunzi.
2. Unaandaa wenyewe, kwa usahihi na kwa haraka, matokeo ya kina, ya aina zote, ya wanafunzi wote waliosajiliwa.
3. Unatuma SMS za Matokeo kwa wazazi. Mzazi mwenye hii app anaweza kufuatilia Matokeo mbalimbali ya mwanae akiwa nyumbani.
4. Mfumo una uwezo wa kuchakata alama za mitihani ya pamoja (joint examinations), kama MOCK nk.. na kuandaa yenyewe kitabu chenye matokeo ya kina ya mtihani huo.
5. Mfumo unatengeneza ratiba ya jumla ya masomo (wenyewe bila msaada). Ratiba inayotengenezwa inazingatia mambo 10 muhimu ikiwemo, kutokuwepo mgongano wa vipindi na mrudio wa vipindi kwa siku, inaonyesha somo na mwalimu anayefundisha na jumla ya vipindi kwa kila mwalimu, imezingatia idadi ya vipindi kwa kila somo kwa wiki nk..
6. Andalio la Somo (Lesson Plan). Mfumo unamuwezesha mwalimu wa somo kuandika (SIO KUANDAA) andalio la somo (lesson plan) kwa haraka sana, muda usiozidi dakika 1.
7. Attendance. Mwalimu wa darasa anaweza kuchukua mahudhurio (Attendance) ya wanafunzi kwa haraka sana. Mwalimu atatumia App kuita majina, app itatengeneza pdf yenye muonekano sawa na attendance register hardcopy. Pia inakokotoa yenyewe wastani wa mahudhurio ya mwezi.
8. Accounting. Mfumo unaweka rekodi za miamala mbalimbali inayoweza kufanyika shuleni kama ada na michango. Unatoa risiti ya malipo (ya shule, sio ya serikali) ambayo inaweza kuprintiwa. Mfumo unakutengenezea wenyewe taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi chochote utakachotaka mf. robo mwaka, nusu mwaka, mwaka au mwezi fulani hadi fulani nk..
9. Taarifa ya mwalimu wa zamu (Duty Book). Mwalimu wa zamu sasa anaweza kuandika ripoti ya zamu kwa haraka zaidi na mkuu wake akaiona na kuisaini taarifa hiyo popote anakapokuwa. Hii inamsaidia kujua kinachoendelea shuleni muda wowote.
10. Mfumo unaonyesha taarifa za usajili wa walimu na wanafunzi kwa idadi kwa kuzingatia jinsi, mikondo nk.. unawezesha kupakua orodha za wanafunzi kimadarasa (class lists (pdf)) kwaajili ya matumizi mbalimbali. Una mazingira rafiki ya kupata kwa haraka taarifa inayohitajika