Soma Quran
Install Now
Soma Quran
Soma Quran

Soma Quran

Tafsiri ya Quran kwa lugha ya kiswahili pamoja na ufafanuzi wake.

Developer: SwahiliTech.net
App Size: 3.8M
Release Date: Aug 2, 2018
Price: Free
4.7
51 Ratings
Size
3.8M

Screenshots for App

Mobile
Tarjama hii imeandaliwa kwa lengo la kuwawezesha wazungumzaji wa Kiswahili kufahamu maana sahihi ya Qur-aan Tukufu, nayo ni ya kwanza ya aina yake kwa kuwa inaendana na manhaj ya Nabiy wetu Muhammad (صلى لله عليه وآله سلم) na Salafus-Swaalih; Maswahaba (رضي الله عنهم), Taabi’iyn na waliowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya mwisho.

Kuna mambo mengi yanayoimaizi Tarjama hii kulinganisha na Tarjama zingine za Kiswahili. Kati ya mambo hayo ni:

Imezithibitisha Sifa za Allaah (سبحانه وتعالى) zinazolaikiana na Utukufu Wake kama Alivyojithibitishia Yeye Mwenyewe na kuthibitishiwa pia na Rasuli Wake (صلى الله عليه آله وسلم) kama Sifa ya ‘Uluww (Kuweko juu), Istiwaa, Kusikia, Kuona, Mikono, Kuzungumza na Sifa nyinginezo zilizothibiti bila kuzifanyia ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala tamthiyl (kumithilisha, kulinganisha), wala takyiyf (kuainisha; namna gani), wala tahriyf (kupotosha na kubadilisha maana), kama vile inavyojulikana katika ‘Aqiydah ya Ahlus Sunnah wal Jamaa’ah..

Imethibitisha masaail yote yahusianayo na mambo yaliyofichika (ghayb) kama Waumini kumwona Rabb wao Siku ya Qiyaamah na Peponi. Pia adhabu ya kaburi, Asw-Swiraatw (Njia ya kuvuka watu Siku ya Qiyaamah), Al-Miyzaan (Mizani) na mengineyo yaliyotajwa kwenye Qur-aan ‘Adhimu.

Tumechagua kwa uangalifu mkubwa misamiati inayowafikiana na makusudio ya Aayah.

Tumefafanua baadhi ya vipengele vinavyohitajia kufafanuliwa kama masaail ya ki-‘Aqiydah na kadhalika.

Tumeweka sababu za kuteremshwa baadhi ya Aayah au Suwrah na mafunzo yanayopatikana.

Tumetaja An-Naasikh (kinachofuta) na Al-Mansuwkh (kinachofutwa) pale tulipoweza.

Kazi yoyote ya mwana Aadam bila shaka haikosi kasoro, nasi kwa Tawfiyq ya Allaah tumejitahidi kiasi cha uwezo wetu kuepuka hilo. Tunamwomba yeyote atakayegundua kosa, au kasoro, au mponyoko wowote ndani ya Tarjama hii, asisite kutujulisha haraka awezavyo, nasi tutashukuru kwa hilo. Atujulishe kupitia barua yetu pepe: [email protected]

Tunamwomba Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Fadhila Zake, Ukarimu Wake, Upaji Wake, na Ihsani Yake, Atutakabalie kazi hii, hakika Yeye ni Mpaji Mno na Mkarimu Mno.
Show More
Show Less
More Information about: Soma Quran
Price: Free
Version: 1.8
Downloads: 10000
Compatibility: Android 4.0.3 and up
Bundle Id: com.blogspot.uislamuwangu.somaquran
Size: 3.8M
Last Update: Aug 2, 2018
Content Rating: Everyone
Release Date: Aug 2, 2018
Content Rating: Everyone
Developer: SwahiliTech.net


Whatsapp
Vkontakte
Telegram
Reddit
Pinterest
Linkedin
Hide