Renti inakupa uhakika wa kuweza kulipa kodi ya pango kwa wakati bila kusababisha kutofautiana au kufarakana na mwenye nyumba wako. Unapokuwa na Renti, utaweza kulipa kodi yako ya pango kidogo kidogo kadri unavyoweza, kuanzia na TSH 1,000 tu, badala ya kulipa kodi yote kwa wakati mmoja. Hii imekuwa suluhisho kwa watu wengi wenye vipato vya kati na chini ambao wanakabiliwa na changamoto ya kulipa kodi kwa mkupuo mmoja.
Kwa kutumia Renti, unaweza kuweka kiasi kidogo kidogo, kinacholingana na kipato chako, hivyo kurahisisha malipo ya kodi bila shinikizo kubwa la kifedha. Unaweza kutumia Renti kupitia app au kwa kuwasiliana na wakala wa Renti aliye karibu na wewe.