GILLY BONNY ONLINE TV, ni chombo cha habari Kilichoanzishwa kwa lengo la kutoa, kutangaza na kuripoti habari, Matukio, na taarifa mbalimbali nchini Tanzania na Nje ikibidi
Tunahakikisha kila habari tunayoripoti ni ya ukweli na uhakika na ina tija kwa jamii na taifa kwa ujumla, Tunafuata misingi ya habari kwa kuripoti habari zenye uwiano na kutoa fursa sawa kwa pande zote bila kuangalia Udini, Ukabila wala ubaguzi.
Tunajiepusha na mambo yoyote yanayoweza kusababisha uchochezi, kuvuruga, kuharibu ama kuhatarisha amani ya mtu, jamii, ama taifa.
Hata hivyo Tunaheshimu Maoni ya kila mtazamaji wetu Lakini hatutaki maoni yenye Matusi, Kejeli, uchochezi na mambo mengine yanakwenda kinyume na maadili, hivyo tuwataka watazamaji wetu kuwa makini na kutoa maoni kwa ustaarabu kwa kuheshimu sheria za nchi.
Ikumbukwe kuwa Kwa Mujibu wa sheria Mwaka 2018 tumepewa Leseni na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, hivyo tunafanya kazi kwa usimamizi wa Mamlaka hiyo, kwa hiyo Mtazamaji wetu yeyote atakayekwenda kinyume na sheria akaingia kwenye matatizo na TCRA au mamlaka nyingine za Kiserikali GILLY BONNY ONLINE TV haitahusika kwa lolote.
Tunapendezwa sana na maoni ya kila Mtazamaji wetu lakini muhimu zaidi ni azingatie staha, ueledi, Heshima, busara na mambo mengine yanakwenda kinyume na Kanuni, taratibu na sheria za nchi.
Aidha Haturuhusu Mtu yeyote kuchungua habari zetu na kuzitumia kwa Malengo yake binafsi bila kutoa Taarifa ama kuwasiliana na Uongozi wa Gilly Bonny Online Tv, tukigundua umefanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa muhusika ikiwemo kudai haki miliki (Copyright, Strike), na kukushtaki kwa Mamlaka husika ama vyombo vya dola.
Kwa namna ya kipekee kabisa tunashukuru kwa kila mdau ambaye amekuwa akitembelea Gilly Bonny Online Tv, tunatambua mchango wako katika tasnia ya habari Tanzania, tunaomba uendelee kutufuatilia zaidi na hata kuwafahamisha ndugu, Jamaa na Marafiki habari njema kuhusu Online Tv yetu.