VIPENGELE MUHIMU
1. Usimamizi wa Bajeti
✅ Kutengeneza/Kuhariri/Kufuta Bajeti
Unaweza kuunda bajeti mpya, kubadilisha bajeti iliyopo, au kuifuta kabisa. Kila bajeti inaweza kuhaririwa wakati wowote.
✅ Kuweka Jina la Bajeti (max maneno 50)
Jina la bajeti linaweza kuwa na herufi 50. App inakuonyesha umebaki na herufi ngapi ukiandika (mfano: 25/50).
✅ Kuweka Kiasi cha Bajeti
Weka jumla ya fedha unazotaka kutumia kwenye bajeti hiyo. Inawekwa kwa shilingi (TZS) na ina format nzuri automatic.
✅ Kuchagua Tarehe ya Kuanza
Chagua siku bajeti yako itakapoanza. Calendar itakuonesha uchague tarehe rahisi.
✅ Kuongeza Matumizi Mengi
Unaweza kuongeza matumizi mengi unavyotaka kwenye bajeti moja. Minimum ni matumizi 1, maximum hakuna.
✅ Kuweka Bajeti Imekamilika
Ukimaliza kutumia bajeti, unaweza imweka "Imekamilika" na itaonekana na badge ya green.
2. Kufuatilia Matumizi
✅ Kuongeza/Kuondoa Matumizi
Unaweza kuongeza matumizi mapya kwenye bajeti yoyote, au kufuta matumizi usiyoyahitaji. Kubadilisha pia kunawezekana.
✅ Majina ya Matumizi (max maneno 40)
Kila matumizi ina jina lake, maximum herufi 40. Character counter inakuambia umebaki na ngapi.
✅ Kiasi cha Matumizi
Weka kiasi cha kila matumizi. Ina format ya shilingi automatic na thousand separators (mfano: 50,000).
✅ Weka Matumizi Yote Completed
Kuna option ya kuweka matumizi yote completed kwa click moja, badala ya kubonyeza moja moja.
✅ Hesabu za Automatic
App inahesabu jumla ya matumizi, baki, na asilimia automatic. Huhitaji kukokotoa calculator!
3. Hali ya Bajeti
✅ Kufuatilia Kiasi Kilichobaki
App inakuonyesha umebaki na kiasi gani cha bajeti yako. Calculation ni automatic (Bajeti - Matumizi = Baki).
✅ Kutambua Bajeti Zimezidi
Kama umetumia zaidi ya bajeti, app inakuambia "Imezidi" na kuonyesha umezidi kiasi gani.
✅ Kuonyesha Asilimia ya Matumizi
Progress bar na percentage inaonyesha umetumia asilimia ngapi ya bajeti (mfano: 75%). Visual na rahisi kuelewa.
✅ Alama ya Bajeti Zilizo Expire (orange)
Bajeti ambazo tarehe ya kuanza imepita lakini bado hazijakamilika zinaonekana na badge ya orange "Imeisha Muda".
✅ Alama ya Bajeti Zilizokamilika (green)
Bajeti ulizozimaliza zinaonekana na badge ya green "Imekamilika". Vizuri kuona progress!
✅ Alama ya Bajeti Zilizozidi (red)
Bajeti ulizozitumia zaidi ya limit zinaonekana na badge ya red "Imezidi". Warning ya kuangalia fedha.
4. Takwimu na Ripoti
✅ Kuchuja kwa Hali
Unaweza chuja bajeti kulingana na hali: Zote, Zimekamilika, Zinaendelea, Zimezidi, au Ndani ya Bajeti. Rahisi kupata unavyotaka.
✅ Kuchuja kwa Tarehe
Chagua tarehe range: Leo, Wiki hii, Mwezi huu, au Custom range. Unaona bajeti za kipindi fulani tu.
✅ Statistics za Muhtasari
Jedwali kubwa la statistics linaonyesha jumla ya bajeti, zipi zimekamilika, zipi zimezidi, na takwimu nyingine muhimu.
✅ Export kwenye PDF na MS WORD
Toa ripoti kamili kwa format ya PDF. Inatengenezwa na sections 3: Muhtasari, Bajeti, na Matumizi. Professional na ready for printing.
✅ Export kwenye CSV/Excel (faili 3)
Toa ripoti kwa format ya CSV (Excel). Faili 3 zitatengenezwa: Muhtasari, Bajeti Records, na Matumizi Records. Unaweza fungua kwenye Excel/Sheets.
✅ Hesabu Sahihi ya JUMLA
JUMLA kwenye ripoti inaonyesha jumla ya bajeti tu, SI bajeti + matumizi. Hesabu sahihi kabisa!
5. Arifa (Notifications)
✅ Arifa ya Bajeti Zinazoanza Leo
Kila siku app inacheki kama kuna bajeti zinazotarajiwa kuanza leo. Inapiga kengele na kukuambia zipo ngapi.
✅ Arifa ya Bajeti Zinazoanza Kesho
App inakuarifu bajeti zinazotarajiwa kuanza kesho ili ujiandae. Message clear na count ya bajeti.
✅ Arifa Mara Moja kwa Siku
Notifications zinapiga mara moja tu kwa siku. Hazitapiga tena baada ya kuona notification ya siku hiyo.
✅ Backup Database kwenye Faili
Unaweza fanya backup ya database yako yote kwenye file ya .db. Hifadhi kwenye phone storage, Google Drive, au popote.
✅ Restore kutoka Backup
Unaweza restore data yako kutoka backup file. Ikiwa umepoteza data au umebadilisha simu, restore na kila kitu kirudi!