Jumuiya Yangu App ni suluhisho la kidijitali lililobuniwa kwa upendo na nia njema ili kuimarisha mshikamano na uwazi ndani ya jamii zetu za kidini na kijamii. Kupitia programu hii, wanajumuiya wanaweza kutoa sadaka, michango ya hiari, au michango ya kila mwezi kwa urahisi, popote walipo, na kwa usalama wa hali ya juu.
Programu hii haina lengo la kibiashara, bali imeandaliwa kama sehemu ya huduma kwa jamii. Inalenga kusaidia familia, makanisa, misikiti, au jumuiya ndogondogo kupata njia rahisi ya kusimamia na kufuatilia sadaka na michango yao bila usumbufu wa karatasi au makaratasi ya michango ambayo hupotea au kuchakaa kwa haraka