Nafasi za kazi 24/7 ni application inayokuwezesha kupata taarifa juu ya nafasi za kazi zinazotolewa kila siku kutoka vyanzo Mbalimbali vya kuaminika. Katika application ya Nafasi za ajira 24/7 utapata updates za uhakika katika simu yako kwa muda wote ndani ya masaa 24 pale nafasi za kazi zinapotolewa. Pia application ya nafasi za kazi 24/7 inakupa uwanja mkubwa wa wewe unayetafuta ajira kupata ajira utakazo kwa uhakika wa chanzo cha ajira bila kukiuka taratibu. Kumbuka! Suala la kupata fursa za ajira ni la bure hivyo, Nafasizakazi24/7 inakuepusha na matapeli ambao wangekuhitaji kulipia ili kupata ajira.