HALA App Cost-Manager Buildings
Install Now
HALA App Cost-Manager Buildings
HALA App Cost-Manager Buildings

HALA App Cost-Manager Buildings

Taarifa za Ujenzi “Kiganjani Mwako” Makazi Bora kwa Gharama Nafuu– HALA App.

Developer: NYAKAME LIMITED
App Size: 3.6M
Release Date: Mar 14, 2020
Price: Free
4.3
6 Ratings
Size
3.6M

Screenshots for App

Mobile
HALA App ni teknolojia ya kupata taarifa za ujenzi katika maeneo yafuatayo; Gharama za ufundi wakati wa ujenzi wa nyumba (Labour Cost), Maombi ya Kujengewa Nyumba, Kujua bei ya soko ya vifaa vya ujenzi (madukani) kwa kila mkoa (Market Price for Construction Materials),Kanuni za jinsi ya kupata Quantity za ujenzi wa nyumba (Measurement of Quantities for building Works), Kupata idadi ya vifaa vinavyohitajika wakati wa ujenzi wa nyumba (Schedule of Materials) .

Gharama za Ufundi Wakati wa Ujenzi wa Nyumba (Labour Cost); kupitia teknolojia hii mtumiaji ataweza kujua gharama (bei) za malipo kwa mafundi wakati wa ujenzi wa nyumba kwa kila hatua ya ujenzi kuanzia kuseti pamoja na kuchimba msingi, kujenga ukuta , kuezeka, kusakafia, kuweka madirisha na milango, kuweka umeme, kuweka maji ndani ya nyumba, kufunga mifumo ya TEHEMA na kutengeneza “garden”. Kupitia teknolojia hii mtumiaji atafahamu gharama (bei) za ujenzi kwa kipimo rahisi ambacho ni idadi ya vyumba anavyotaka kujenga, n.k. Baada ya kufahamu gharama (bei) hizo za ujenzi, Mtumiaji atapata huduma hiyo ya kujengewa nyumba kulingana na gharama (bei) pendekezi. Mteja atapata faida ya kupata usimamizi (maana yake kazi yake itakuwa na mwangalizi mwingine mbali na fundi hasa kwa wale wateja wanaojenga nyumba zao za makazi ambazo sio gorofa wala za biashara na hawana uwezo wa kuajiri “consultant”) na uhakika wa fedha zake kutopetea (kutapeliwa) na fundi kwa kuwa malipo yatafanyika kupitia mfumo huu wa HALA App.

Maombi ya Kujengewa Nyumba, kupitia teknolojia hii mtumiaji anaweza kutuma maombi ya kujengewa nyumba nzima kwa kutuma taarifa ya aina ya nyumba anayotaka kujengewa, kuainisha idadi ya vyumba , eneo alilopo na maelezo mengine.

Kujua Bei ya Soko ya Vifaa vya Ujenzi (Madukani) kwa kila Mkoa (Market Price for Construction Materials); kupitia teknolojia hii, mtumiaji anaweza kupata bei ya soko ya vifaa vya ujenzi bila kuanza kupiga simu au kwenda kuuliza madukani, vifaa vya ujenzi , hasa anapokuwa anajenga eneo ambalo kwa sasa haishi huko. Lakini pia teknolojia hii itawasaidia wauzaji wa vifaa vya ujenzi kutangaza vifaa kirahisi na kujipanua katika kufahamika pamoja na kuongeza soko. Wajenzi wengi wa nyumba wamekuwa wakipoteza pesa nyingi wakati wa ununuzi wa vifaa vya ujenzi wa nyumba kwa kudaganywa bei na wale wanaowatuma kununua vifaa vya ujenzi hasa pale wao wanapokuwa na majukumu mengine ya kusimamia au kutekeleza . Kupitia mfumo huu sasa mtumiaji atapata bei ya bidhaa za ujenzi popote kwa kuunganishwa na maduka yanayouza vifaa hivyo vya ujenzi pamoja na bei zake. Na kizuri nikwamba kupitia mfumo huu mtumiaji anaweza kupiga simu na kuagiza mumililiki wa duka kumuletea bidhaa za ujenzi mahali yeye mteja alipo.

Kanuni za jinsi ya kupata “Quantity” za ujenzi wa nyumba, kupitia teknolojia hii mtumiaji atapata kanuni za jinsi ya kupata “Quantity” za ujenzi , hii itamurahisishia mtumiaji kupata mwongozo sahihi wa jinsi ya kupata Quantity kwa kufuata taratibu za “Standard methods for Measurements of Building Works For East Africa” .

Kupata Idadi ya Vifaa Vinavyohitajika Wakati wa Ujenzi wa Nyumba (Schedule of Materials); kupitia teknolojia hii , mtumiaji anaweza kujua idadi ya vifaa vya ujenzi kwa kila sehemu (Elements of Building) ya ujenzi wa nyumba kama vile idadi ya simenti , mchanga, kokoto, matofali, rangi, mbao za kuezekea, mbao za dari, mabati, malumalu (tiles) n.k. Anachotakiwa kufanya mtumiaji ni kutafuta “Quantity” kupitia kwenye mchoro wa nyumba yake na kuziingiza kwenye mfumo huu, kwa mfano ; ukiingiza eneo la kujenga ukuta {mita za mraba 20 (20m2)}, mfumo utakupa idadi ya matofali, Mchanga na simenti kwa hilo eneo uliloingiza kwenye mfumo. Sehemu hii inafaa sana kutumiwa na wataalam wote katika sekta ya ujenzi hasa (Technicians, Engineers, Architects na Contractors)

Karibu Tukuhudumie –HALA App: NYAKAME LIMITED} www.nyakame.co.tz
Show More
Show Less
More Information about: HALA App Cost-Manager Buildings
Price: Free
Version: 2.1
Downloads: 100
Compatibility: Android 4.0.3 and up
Bundle Id: com.nyakame.app
Size: 3.6M
Last Update: Mar 14, 2020
Content Rating: Everyone
Release Date: Mar 14, 2020
Content Rating: Everyone
Developer: NYAKAME LIMITED


Whatsapp
Vkontakte
Telegram
Reddit
Pinterest
Linkedin
Hide