Kanisa Langu ni app ya kidigitali inayorahisisha usimamizi na uendeshaji wa shughuli mbalimbali ndani ya kanisa. App hii imebuniwa ili kuraratibu na kusimamia shughuli zote za kanisa kuanzia ngazi ya Dayosisi, Jimbo, Usharika, Mitaa, Jumuiya hadi kwenye Idara na Vikundi mbalimbali.
Kupitia Kanisa Langu, kanisa linaimarisha ufanisi wa utendaji kazi, kuongeza uwajibikaji na uwazi, na kurahisisha upatikanaji wa taarifa muhimu kwa wakati, hivyo kusaidia viongozi na waumini kufanya maamuzi kwa wepesi, uharaka na usahihi.