Bembea ya Maisha ni hadithi kuhusu Yona na mkewe Sara pamoja na Bunju na mkewe Neema. Wahusika hawa wanajikuta katika vuta n’kuvute inayochochewa na mitazamo ya kitamaduni, uhalisia wa mambo pamoja na matamanio ya wahusika binafsi. Baina yao kuna mitikiso inayotishia familia, ndoa na mahusiano ya kijamii. Kuna shutma, shaka, tuhuma na mivutano. Lakini pia kuna hongera, imani, ushirikiano, upendo, kutanabahi na mshikamano. Katika huu mseto wa mambo ipo sauti imara ya Sara inayosikika ikihimiza na kuzindua. Sauti inayoiona kila hali mfano wa bembea. 
Mwongozo wa Bembea ya Maisha  utakupa tu mwelekeo  lakini sharti kusoma vitabu vingine.
Ushauri muhimu kwa mtahiniwa.
1) Mtahiniwa sharti asome kitabu husika (Bembeaya Maisha) barabara na  kukielewa.  
2) Mwongozo ni kurunzi ya kumulikia njia, kwa hivyo, mtahiniwa sharti aelewe  aendako.  
3) Ni muhimu kusoma na kulielewa swali lililoulizwa. Ni vyema kujiuliza swali  lifuatalo: Mtahini anataka habari gani kutokana na swali hili?  
4) Usitoke nje ya muktadha wa swali na kuandaa habari ambazo hazihusiani na  swali uliloulizwa.  
5) Ikiwezekana, toa mifano kutoka kwenye tamthilia inayohusiana na jambo  unalolifafanua ili kuweka jambo hilo wazi.