Nyimbo za Kristo ni program iliyo na nakala za nyimbo za kiswahili kama zilivyochapwa na Tanzania Adventist Press(TAP). Nyimbo hizi ni nzuri na zinaweza somwa na mtu yeyote pasipo kubagua umri wala dini. Karibu tumwabudu Mungu kwa njia ya nyimbo pasipo usumbufu wa matangazo.
Zekaria 2:10 BHN
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Enyi watu wa Siyoni, imbeni na kufurahi kwa kuwa ninakuja na kukaa kati yenu.
Sifa za Program
- Inakuwezesha kusoma nyimbo pasipo intaneti.
- Inakuwezesha kutafuta wimbo kwa maneno au namba.
- Wezesha mwanga wa simu kutozima pindi usomapo.
- Weka nyimbo unazozipenda kwenye orodha ya nyimbo pendwa.
- Badili ukubwa wa maneno.
- Pangilia nyimbo kwa namba au alfabeti.