Tenzi za Rohoni- Swahili Hymns – Nyimbo za Kuabudu na kusifu kiganjani mwako
App hii itakusaidia kupata nyimbo kutoka katika kitabu cha Tenzi. Iwe ni kwa ajili ya ibada, maombi ya kibinafsi, makongamano au wakati wa kutafakari Neno la Mungu, unaweza kusoma maneno ya wimbo, na hata kushiriki na wengine maneno ya nyimbo.
Tenzi za Rohoni- Swahili Hymns, ina sifa muhimu zilizoundwa kukuhudumia kikamilifu. Unapata nyimbo Tenzi zenye uwezo wa kuzisoma hata nje ya mtandao, unaweza kutumia alama ya utafutaji yaani (search icon) kupata wimbo unaohitaji kwa haraka. Sifa nyingine ni pamoja na kuweka nyimbo unazozipenda kwenye orodha maalum (favorites/Bookmark), kutumia hali ya giza an rangi tofauti (theme colors), na kushiriki maneno ya wimbo na marafiki au familia kupitia mitandao ya kijamii. Muundo wa unarahisisha matumizi kwa kila mtu.
Pakua Tenzi za Rohoni - Swahili Hymns leo na ufurahie wingi wa baraka kupitia nyimbo hizi za kiroho. Fanya maisha yako ya maombi kuwa ya kupendeza zaidi na ujaze moyo wako na amani ya Kristo. App hii ni mahususi kwa wakristo wote, waimbaji, na watumishi wa Mungu, hata mtu yeyote anayependa nyimbo za kusifu na kuabudu. Tunakuombea Roho mtakatifu akakusaidie kuhisi uwepo wa Mungu kupitia nyimbo zenye ujumbe mzito na wenye baraka.
Ipakue sasa na Usisite kupendekeza app hii kwa watu unaowapenda,