Nyimbo za KKKT ni App iliyokusanya nyimbo zote 440 kutoka kitabu cha kilutheri yaani Mwimbieni Bwana, Programu hii imetengenezwa kwa ajili ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri, kwaya, na Wakristo wote wanaopenda kusifu na kumwabudu Mungu kupitia nyimbo za imani. Ukiwa na programu hii, nyimbo zote zipo mkononi mwako popote ulipo.
App hii Haina Liturgia wala kalenda ni Nyimbo Tu kutoka katika vitabu va kilutheri
Ndani ya App utapata nyimbo zote zikiwa zimeandikwa kwa mpangilio mzuri, rahisi kusoma na kufuata wakati wa ibada au au jumuiya. Pia kuna kipengele cha kutafuta nyimbo kwa namba au jina, hivyo huna haja ya kupitia ukurasa kwa ukurasa. Ikiwa kuna nyimbo unazopenda zaidi, unaweza kuziweka kwenye orodha ya vipendwa ili uzifikie haraka wakati wowote. App hii hii pia hufanya kazi bila intaneti, hivyo unaweza kutumia nyimbo zako hata ukiwa maeneo yasiyo na mtandao.
App ya Nyimbo za KKKT inalenga kukupeleka karibu zaidi na Mungu kwa kurahisisha ibada na ushirika. Iwe ni kanisani, nyumbani, au katika mikutano ya kwaya na jumuiya, unaweza kufungua app hii na kuimba kwa pamoja kwa moyo wa ibada. Aidha, Nyimbo za KKKT App imeundwa kwa mwonekano rahisi na maandiko makubwa, ili kila mtu aweze kusoma vizuri na kushiriki katika sifa na kuabudu bila usumbufu.
⚠️ Kumbuka: Hii siyo programu rasmi ya KKKT. Imetengenezwa kwa lengo la kusaidia waumini kupata nyimbo tu kwa urahisi zaidi. Yaliyomo yanatokana na vitabu vya nyimbo Mwimbieni Bwana vinavyotumika katika makanisa Kilutheri. App hii ni msaada wa kiroho kwa waumini na jumuiya na kwaya na watu wanaopenda kumtumikia Mungu kupitia nyimbo za kusifu na kuabudu.
Ila usisahau kubeba kitabu cha Nyimbo yaani TMW ukienda ibadani jumapili, App hii itakusaidia kama mbadala tu kwa Nyimbo pekee.
Kumbuka kwenda na Kitabu Cha TUMWABUDU MUNGU WETU au Pakua App ya TMW kwa ajili ya Liturgia na Kalenda ya Mwaka.