App hii ya Kilimo na Mifugo ni kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo na ufugaji na namna ya kupambana na magonjwa ya kilimo na mifugo. Maswali yote ya kilimo na mifugo yanayowasumbua wakulima na wafugaji sehemu mbalimbali za nchi yatapatiwa majibu kupitia app hii. Fuatilia kila siku ili upate elimu bora kabisa ya kilimo na ufugaji, ulime na ufuge kwa kufuata kanuni na mbinu za kisasa zinazotumiwa duniani kote. Hakika hapa utapata elimu ya kilimo na ufugaji bure kabisa na usisite kuwashirkisha wengine nao wafaidi elimu ya bure.